1 Corinthians 10:5-10
5 aLakini Mungu hakupendezwa na wengi wao, kwa hiyo miili yao ilitapakaa jangwani.6 bBasi mambo haya yalitokea kama mifano ili kutuzuia tusiweke mioyo yetu katika mambo maovu kama wao walivyofanya. 7 cMsiwe waabudu sanamu, kama baadhi yao walivyokuwa, kama ilivyoandikwa, “Watu waliketi chini kula na kunywa, kisha wakainuka kucheza na kufanya sherehe za kipagani.” 8 dWala tusifanye uzinzi kama baadhi yao walivyofanya, wakafa watu 23,000 kwa siku moja. 9 eWala tusimjaribu Kristo, kama baadhi yao walivyofanya, wakafa kwa kuumwa na nyoka. 10 fMsinungʼunike kama baadhi yao walivyofanya, wakaangamizwa na mharabu.
Copyright information for
SwhNEN