1 Chronicles 6:31-39
Waimbaji Wa Hekalu
31 aHawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya Bwana, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko. 32Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Solomoni alipojenga Hekalu la Bwana huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.33 bWafuatao ni watu waliohudumu pamoja na wana wao:
Kutoka ukoo wa Kohathi walikuwa:
Hemani, mpiga kinanda,
alikuwa mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli,
34 cmwana wa Elikana, mwana wa Yerohamu,
mwana wa Elieli, mwana wa Toa,
35mwana wa Sufu, mwana wa Elikana,
mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai,
36mwana wa Elikana, mwana wa Yoeli,
mwana wa Azaria, mwana wa Sefania,
37 dmwana wa Tahathi, mwana wa Asiri,
mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora,
38 emwana wa Ishari, mwana wa Kohathi,
mwana wa Lawi, mwana wa Israeli;
39 fna msaidizi wa Hemani alikuwa Asafu, aliyesimama mkono wa kuume:
Asafu mwana wa Berekia, mwana wa Shimea,
Copyright information for
SwhNEN