‏ 1 Chronicles 6:27-34

27 aNahathi akamzaa Eliabu,
Eliabu akamzaa Yerohamu, Yerohamu akamzaa Elikana,
Elikana akamzaa Samweli.
28 bWana wa Samweli walikuwa:
Yoeli mzaliwa wake wa kwanza,
na Abiya mwanawe wa pili.
29Wafuatao ndio wazao wa Merari:
Merari akamzaa Mahli, Mahli akamzaa Libni,
Libni akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Uza,
30Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia,
Hagia akamzaa Asaya.

Waimbaji Wa Hekalu

31 cHawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya Bwana, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko. 32Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Solomoni alipojenga Hekalu la Bwana huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.

33 dWafuatao ni watu waliohudumu pamoja na wana wao:

Kutoka ukoo wa Kohathi walikuwa:
Hemani, mpiga kinanda,
alikuwa mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli,
34 emwana wa Elikana, mwana wa Yerohamu,
mwana wa Elieli, mwana wa Toa,
Copyright information for SwhNEN