1 Chronicles 29:9-17
9 aWatu wakafurahi kwa sababu ya itikio la hiari la viongozi wao, kwa kuwa walikuwa wametoa kwa hiari na kwa moyo wote kwa Bwana. Mfalme Daudi pia akafurahi sana.Maombi Ya Daudi
10 bDaudi akamhimidi Bwana mbele ya kusanyiko lote, akisema:“Uhimidiwe wewe, Ee Bwana,
Mungu wa Israeli baba yetu,
tangu milele hata milele.
11 cUkuu na uweza, ni vyako, Ee Bwana,
na utukufu na enzi na uzuri,
kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani
ni chako wewe.
Ee Bwana, ufalme ni wako;
umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote.
12 dUtajiri na heshima vyatoka kwako;
wewe ndiwe utawalaye vitu vyote.
Mikononi mwako kuna nguvu na uweza
ili kuinua na kuwapa wote nguvu,
13Sasa, Mungu wetu, tunakushukuru
na kulisifu Jina lako tukufu.
14“Lakini mimi ni nani, nao watu wangu ni nani, hata tuweze kukutolea kwa ukarimu namna hii? Vitu vyote vyatoka kwako, nasi tumekutolea tu vile vitokavyo mkononi mwako. 15 eSisi ni wageni na wapitaji machoni pako, kama walivyokuwa baba zetu wote. Siku zetu duniani ni kama kivuli, bila tumaini. 16Ee Bwana Mungu wetu, kwa wingi wote huu ambao tumekutolea kwa kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina lako Takatifu, vimetoka mkononi mwako, navyo vyote ni mali yako. 17 fNinajua, Mungu wangu, kwamba wewe huujaribu moyo na unapendezwa na unyofu. Vitu hivi vyote nimetoa kwa hiari na kwa moyo mnyofu. Nami sasa nimeona kwa furaha jinsi watu wako walioko hapa kwa hiari yao walivyokutolea wewe.
Copyright information for
SwhNEN