1 Chronicles 14:8-17
Daudi Awashinda Wafilisti
(2 Samweli 5:17-25)
8 aWafilisti waliposikia kuwa Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli yote, wakapanda na jeshi lao lote kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari hizo, naye akatoka ili kwenda kukabiliana nao. 9 bBasi Wafilisti walikuwa wameingia na kushambulia Bonde la Warefai, 10Hivyo Daudi akamuuliza Mungu: “Je, niende kuwashambulia hao Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?”Bwana akamjibu, “Nenda, nitawatia mikononi mwako.”
11 cHivyo Daudi pamoja na watu wake wakakwea mpaka Baal-Perasimu, ▼
▼Maana yake ni Bwana Afurikae.
akawashinda huko. Akasema, “Kama maji yafurikavyo, Mungu amewafurikia adui zangu kwa kutumia mkono wangu.” Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Baal-Perasimu. 12 eWafilisti walikuwa wameacha miungu yao huko, Daudi akaamuru iteketezwe kwa moto. 13 fKwa mara nyingine Wafilisti wakavamia lile bonde; 14 ghivyo Daudi akamuuliza Mungu tena, naye Mungu akamjibu, “Usiwapandie moja kwa moja, bali wazungukie na uwashambulie kutoka mbele ya hiyo miti ya miforosadi. 15Mara usikiapo sauti ya kwenda juu ya hiyo miti ya miforosadi, hapo ndipo utoke upigane vita, kwa sababu hiyo itaonyesha kwamba Mungu amekutangulia ili kupiga jeshi la Wafilisti.” 16 hKwa hiyo Daudi akafanya kama alivyoagizwa na Mungu, wakalipiga jeshi la Wafilisti kuanzia Gibeoni hadi Gezeri.
17 iHivyo umaarufu wa Daudi ukaenea katika kila nchi, naye Bwana akayafanya mataifa yote kumwogopa Daudi.
Copyright information for
SwhNEN