1 Chronicles 14:1-7
Nyumba Ya Daudi Na Jamaa Yake
(2 Samweli 5:11-16)
1 aBasi Hiramu mfalme wa Tiro akawatuma wajumbe kwa Daudi, wakiwa na magogo ya mierezi, waashi na maseremala ili kumjengea jumba la kifalme. 2 bNaye Daudi akatambua kwamba Bwana amemwimarisha kuwa mfalme juu ya Israeli na kwamba ufalme wake umetukuzwa kwa ajili ya Israeli, watu wake.3 cHuko Yerusalemu Daudi akaoa wake wengine zaidi na akawa baba wa wana na mabinti wengi. 4 dHaya ndiyo majina ya watoto waliozaliwa kwake huko: Shamua, Shobabu, Nathani, Solomoni, 5Ibihari, Elishua, Elpeleti, 6Noga, Nefegi, Yafia, 7Elishama, Beeliada na Elifeleti.
Copyright information for
SwhNEN