‏ 1 Chronicles 1:34-42

Wazao Wa Sara

34 aAbrahamu alikuwa baba wa Isaki.
Wana wa Isaki walikuwa:
Esau na Israeli.

Wana Wa Esau

(Mwanzo 36:1-19)

35 bWana wa Esau walikuwa:
Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora.
36 cWana wa Elifazi walikuwa:
Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi;
Elifazi kwa Timna akamzaa Amaleki.
37 dWana wa Reueli walikuwa:
Nahathi, Zera, Shama na Miza.

Watu Wa Seiri Waliokuwa Edomu

(Mwanzo 36:20-30)

38 eWana wa Seiri walikuwa:
Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani.
39 fWana wa Lotani walikuwa wawili:
Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna.
40 gWana wa Shobali walikuwa:
Alvani,
Maandishi ya Kiebrania yanamwita Alian.
Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.
Wana wa Sibeoni walikuwa:
Aiya na Ana.
41 iMwana wa Ana alikuwa:
Dishoni.
Nao wana wa Dishoni walikuwa:
Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.
42Wana wa Eseri walikuwa:
Bilhani, Zaavani na Akani.
Wana wa Dishani walikuwa:
Usi na Arani.
Copyright information for SwhNEN