‏ Song of Solomon 7

1 aEe binti wa mwana wa mfalme,
tazama jinsi inavyopendeza miguu yako katika viatu!
Miguu yako yenye madaha ni kama vito vya thamani,
kazi ya mikono ya fundi stadi.
2Kitovu chako ni kama bilauri ya mviringo
ambayo kamwe haikosi divai iliyochanganywa.
Kiuno chako ni kichuguu cha ngano
kilichozungukwa kwa yungiyungi.
3 bMatiti yako ni kama wana-paa wawili,
mapacha wa paa.
4 cShingo yako ni kama mnara wa pembe ya ndovu.
Macho yako ni vidimbwi vya Heshboni
karibu na lango la Beth-Rabi.
Pua lako ni kama mnara wa Lebanoni
ukitazama kuelekea Dameski.
5 dKichwa chako kinakuvika taji kama mlima Karmeli.
Nywele zako ni kama zulia la urujuani;
mfalme ametekwa na mashungi yake.
6 eTazama jinsi ulivyo mzuri na unavyopendeza,
ee pendo, kwa uzuri wako!
7 fUmbo lako ni kama la mtende,
nayo matiti yako kama vishada vya matunda.
8 gNilisema, “Nitakwea mtende,
nami nitayashika matunda yake.”
Matiti yako na yawe kama vishada vya mzabibu,
harufu nzuri ya pumzi yako kama matofaa,
9 hna kinywa chako kama divai
bora kuliko zote.
Mpendwa

Divai na iende moja kwa moja hadi kwa mpenzi wangu,
ikitiririka polepole juu ya midomo na meno.
10 iMimi ni mali ya mpenzi wangu,
nayo shauku yake ni juu yangu.
11Njoo, mpenzi wangu, twende mashambani,
twende tukalale huko vijijini.
12 jHebu na twende mapema
katika mashamba ya mizabibu
tuone kama mizabibu imechipua,
kama maua yake yamefunguka,
na kama mikomamanga imetoa maua:
huko nitakupa penzi langu.
13 k lMitunguja hutoa harufu zake nzuri,
kwenye milango yetu kuna matunda mazuri,
mapya na ya zamani,
ambayo nimekuhifadhia wewe,
mpenzi wangu.
Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.

Everyone uses cookies. We do too! Cookies are little bits of information stored on your computer which help us give you a better experience. You can find out more by reading the STEPBible cookie policy.