‏ Psalms 123

Kuomba Rehema

Wimbo wa kwenda juu.

1 aNinayainua macho yangu kwako,
kwako wewe ambaye kiti chako cha enzi kiko mbinguni.
2 bKama vile macho ya watumwa
yatazamavyo mkono wa bwana wao,
kama vile macho ya mtumishi wa kike
yatazamavyo mkono wa bibi yake,
ndivyo macho yetu yamtazamavyo Bwana Mungu wetu,
mpaka atakapotuhurumia.

3Uturehemu, Ee Bwana, uturehemu,
kwa maana tumevumilia dharau nyingi.
4Tumevumilia dhihaka nyingi kutoka kwa wenye kiburi,
dharau nyingi kutoka kwa wenye majivuno.
Copyright information for SwhNEN