‏ Psalms 116

Shukrani Kwa Kuokolewa Kutoka Mauti

1 aNinampenda Bwana kwa maana amesikia sauti yangu;
amesikia kilio changu ili anihurumie.
2 bKwa sababu amenitegea sikio lake,
nitamwita siku zote za maisha yangu.

3 cKamba za mauti zilinizunguka,
maumivu makuu ya kuzimu yalinipata,
nikalemewa na taabu na huzuni.
4 dNdipo nikaliitia jina la Bwana:
“Ee Bwana, niokoe!”

5 e Bwana ni mwenye neema na haki,
Mungu wetu ni mwingi wa huruma.
6 f Bwana huwalinda wanyenyekevu,
nilipokuwa katika shida kubwa, aliniokoa.

7 gEe nafsi yangu, tulia tena,
kwa kuwa Bwana amekuwa mwema kwako.
8 hKwa kuwa wewe, Ee Bwana,
umeniokoa nafsi yangu na mauti,
macho yangu kutokana na machozi,
miguu yangu kutokana na kujikwaa,
9 iili niweze kutembea mbele za Bwana,
katika nchi ya walio hai.
10 jNiliamini, kwa hiyo nilisema,
“Mimi nimeteseka sana.”
11 kKatika taabu yangu nilisema,
“Wanadamu wote ni waongo.”

12 lNimrudishie Bwana nini
kwa wema wake wote alionitendea?
13 mNitakiinua kikombe cha wokovu
na kulitangaza jina la Bwana.
14 nNitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana
mbele za watu wake wote.

15 oKifo cha watakatifu kina thamani
machoni pa Bwana.
16 pEe Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako,
mimi ni mtumishi wako,
mwana wa mjakazi wako;
Au: mwanao mwaminifu.

umeniweka huru
toka katika minyororo yangu.

17 rNitakutolea dhabihu ya kukushukuru
na kuliita jina la Bwana.
18 sNitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana
mbele za watu wake wote,
19 tkatika nyua za nyumba ya Bwana,
katikati yako, ee Yerusalemu.

Msifuni Bwana.
Copyright information for SwhNEN