‏ Proverbs 28

1 aMtu mwovu hukimbia ingawa hakuna yeyote anayemfukuza,
bali wenye haki ni wajasiri kama simba.

2Wakati nchi inapokuwa na uasi, inakuwa na viongozi wengi,
bali mwenye ufahamu na maarifa hudumisha utaratibu.

3 bMtu maskini amwoneaye yeye aliye maskini zaidi
ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza mazao.

4 cWale waiachao sheria huwasifu waovu,
bali wale waishikao sheria huwapinga.

5 dWatu wabaya hawaelewi haki,
bali wale wamtafutao Bwana wanaielewa kikamilifu.

6 eAfadhali maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama
kuliko tajiri ambaye njia zake ni potovu.

7 fYeye ashikaye sheria ni mwana mwenye ufahamu,
bali rafiki wa walafi humwaibisha baba yake.

8 gYeye aongezaye utajiri wake kwa riba kubwa mno
hukusanya kwa ajili ya mwingine,
ambaye atawahurumia maskini.

9 hKama mtu yeyote akikataa kusikia sheria,
hata maombi yake ni chukizo.

10 iYeye ambaye humwongoza mwenye haki kwenye mapito mabaya,
ataanguka kwenye mtego wake mwenyewe,
bali wasio na lawama watapokea urithi mwema.

11Mtu tajiri anaweza kuwa na hekima machoni pake mwenyewe,
bali mtu maskini mwenye ufahamu atamfichua.

12 jMwenye haki ashindapo, kuna furaha kubwa,
bali waovu watawalapo, watu hujificha.

13 kYeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa,
bali yeyote aziungamaye na kuziacha hupata rehema.

14 lAmebarikiwa mtu ambaye siku zote humcha Bwana,
bali yeye afanyaye moyo wake kuwa mgumu
huangukia kwenye taabu.

15Kama simba angurumaye au dubu ashambuliaye,
ndivyo alivyo mtu mwovu atawalaye wanyonge.

16Mtawala dhalimu hana akili,
bali yeye achukiaye mapato ya udhalimu
atafurahia maisha marefu.

17 mMtu mwenye kusumbuliwa na hatia ya kuua
atakuwa mtoro mpaka kufa;
mtu yeyote na asimsaidie.

18 nYeye ambaye mwenendo wake hauna lawama
hulindwa salama,
bali yeye ambaye njia zake ni potovu
ataanguka ghafula.

19 oYeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele,
bali yule afuataye mambo ya upuzi atakuwa na umaskini wa kumtosha.

20 pMtu mwaminifu atabarikiwa sana,
bali yeye atamaniye kupata utajiri kwa haraka
hataacha kuadhibiwa.

21 qKuonyesha upendeleo si vizuri,
hata hivyo mtu atafanya kosa kwa kipande cha mkate.

22 rMtu mchoyo ana tamaa ya kupata utajiri,
naye hana habari kuwa umaskini unamngojea.

23 sYeye amkemeaye mtu mwishoni hupata kibali zaidi,
kuliko mwenye maneno ya kusifu isivyostahili.

24 tYeye amwibiaye babaye au mamaye
na kusema, “Si kosa,”
yeye ni mwenzi wa yule aharibuye.

25 uMtu mwenye tamaa huchochea fitina,
bali yule amtegemeaye Bwana atafanikiwa.

26 vYeye ajitumainiaye mwenyewe ni mpumbavu,
bali yeye atembeaye katika hekima hulindwa salama.

27 wYeye ampaye maskini
hatapungukiwa na kitu chochote,
bali yeye awafumbiaye maskini macho
hupata laana nyingi.

28 xWakati waovu watawalapo,
watu huenda mafichoni,
bali waovu wanapoangamia,
wenye haki hufanikiwa.
Copyright information for SwhNEN