‏ Proverbs 1

Utangulizi: Kusudi Na Kiini

1 aMithali za Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli:

2Kwa kupata hekima na nidhamu;
kwa kufahamu maneno ya busara;
3 bkwa kujipatia nidhamu na busara,
kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea;
4 chuwapa busara wajinga,
maarifa na akili kwa vijana;
5 dwenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao,
wenye kupambanua na wapate mwongozo;
6 ekwa kufahamu mithali na mifano,
misemo na vitendawili vya wenye hekima.

7 fKumcha Bwana ndicho chanzo cha maarifa,
lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.

Onyo Dhidi Ya Ushawishi Wa Marafiki Waovu

8 gMwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako,
wala usiyaache mafundisho ya mama yako.
9 hHayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako,
na mkufu wa kuipamba shingo yako.

10 iMwanangu, kama wenye dhambi wakikushawishi,
usikubaliane nao.
11 jKama wakisema, “Twende tufuatane;
tukamvizie mtu na kumwaga damu,
njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia;
12 ktuwameze wakiwa hai kama kaburi,
Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.

wakiwa wazima kama wale wanaotumbukia shimoni.
13Tutapata aina zote za vitu vya thamani
na kujaza nyumba zetu kwa nyara.
14 mNjoo ushirikiane nasi,
vitu vyote tutakavyopata tutagawana.”
15 nMwanangu, usiandamane nao.
Usiweke mguu wako katika njia zao,
16 okwa kuwa miguu yao hukimbilia kwenye dhambi,
ni wepesi kumwaga damu.
17Tazama ni jinsi gani ilivyo kazi bure kutandaza wavu
wakati ndege wote wanakuona!
18 pWatu hawa huvizia kumwaga damu yao wenyewe;
hujivizia tu wenyewe!
19 qHuu ndio mwisho wa wote ambao wanajipatia mali kwa hila;
huuondoa uhai wa wale wenye mali.

Onyo Dhidi Ya Kukataa Hekima

20 rHekima huita kwa sauti kuu barabarani,
hupaza sauti yake kwenye viwanja vikubwa;
21kwenye makutano ya barabara za mji
zenye makelele mengi hupaza sauti,
kwenye malango ya mji hutoa hotuba yake:

22 s“Enyi wajinga, mtangʼangʼania ujinga wenu hadi lini?
Mpaka lini wenye mizaha watafurahia mizaha,
na wapumbavu kuchukia maarifa?
23 tKama mngekuwa mmeitikia karipio langu,
ningekuwa nimemimina roho yangu kwenu
na kuwafahamisha maneno yangu.
24 uLakini kwa kuwa mlinikataa nilipowaita
na hakuna yeyote aliyekubali
niliponyoosha mkono wangu,
25 vkwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote
na hamkukubali karipio langu,
26 wmimi nami nitawacheka katika maafa yenu,
nitawadhihaki wakati janga litawapata:
27 xwakati janga litawapata kama tufani,
wakati maafa yatawazoa kama upepo wa kisulisuli,
wakati dhiki na taabu zitawalemea.

28 y“Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu;
watanitafuta lakini hawatanipata.
29 zKwa kuwa walichukia maarifa,
wala hawakuchagua kumcha Bwana,
30 aakwa kuwa hawakukubali mashauri yangu,
na kukataa maonyo yangu,
31 abwatakula matunda ya njia zao,
na watashibishwa matunda ya hila zao.
32 acKwa kuwa ukaidi wa wajinga utawaua,
nako kuridhika kwa wajinga kutawaangamiza.
33 adLakini yeyote anisikilizaye ataishi kwa usalama,
atatulia, bila kuwa na hofu ya madhara.”
Copyright information for SwhNEN