‏ Numbers 34

Mipaka Ya Kanaani

1 Bwana akamwambia Mose, 2 a“Waamuru Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia nchi ya Kanaani, nchi ambayo itagawanywa kwenu kama urithi itakuwa na mipaka ifuatayo:

3 b“ ‘Upande wenu wa kusini utajumuisha sehemu ya Jangwa la Sini kufuata mpaka wa Edomu. Upande wa mashariki mpaka wenu wa kusini utaanzia mwisho wa Bahari ya Chumvi,
Yaani Bahari Mfu.
4 dkatiza kusini mwa Pito la Akrabimu, endelea mpaka Sini na kwenda kusini ya Kadesh-Barnea. Kisha mpaka huo utaenda hadi Hasar-Adari hadi Azmoni, 5 emahali ambapo utapinda, na kuunganika na Kijito cha Misri na kumalizikia kwenye Bahari ya Kati.
Yaani Mediterania.


6 g“ ‘Mpaka wenu wa magharibi utakuwa Bahari ya Kati. Huu utakuwa mpaka wenu upande wa magharibi.

7 h“ ‘Kwa mpaka wenu wa kaskazini, wekeni alama kuanzia Bahari ya Kati hadi mlima Hori, 8 ina kutoka mlima Hori hadi Pito la Hamathi. Kisha mpaka utaenda hadi Sedadi, 9 jkuendelea hadi Zifroni, na kuishia Hasar-Enani. Huu utakuwa mpaka wenu upande wa kaskazini.

10 k“ ‘Kwa mpaka wenu wa mashariki, wekeni alama kuanzia Hasar-Enani hadi Shefamu. 11 lMpaka utaelekea kusini kuanzia Shefamu hadi Ribla upande wa mashariki wa Aini, na kuendelea kwenye miteremko mashariki mwa Bahari ya Kinerethi.
Yaani Bahari ya Galilaya.
12Kisha mpaka utashuka kuelekea Mto Yordani na kuishia katika Bahari ya Chumvi.

“ ‘Hii itakuwa nchi yenu, ikiwa na mipaka yake kila upande.’ ”

13 nMose akawaamuru Waisraeli: “Gawanyeni nchi hii kwa kura kama urithi. Bwana ameagiza kwamba itolewe kwa yale makabila tisa na nusu, 14 okwa sababu jamaa ya kabila la Reubeni, kabila la Gadi, na nusu ya kabila la Manase wamekwishapokea urithi wao. 15Haya makabila mawili na nusu wamekwishapokea urithi wao upande wa mashariki wa Yordani ngʼambo ya Yeriko, kuelekea mawio ya jua.”

16 Bwana akamwambia Mose, 17 p“Haya ndiyo majina ya watu ambao watakusaidia kugawanya nchi kama urithi: Eleazari kuhani na Yoshua mwana wa Nuni. 18 qTena uteue kiongozi mmoja kutoka kila kabila kusaidia kuigawanya nchi. 19 rHaya ndiyo majina yao:

“Kalebu mwana wa Yefune,
kutoka kabila la Yuda;
20 sShemueli mwana wa Amihudi,
kutoka kabila la Simeoni;
21 tElidadi mwana wa Kisloni,
kutoka kabila la Benyamini;
22Buki mwana wa Yogli,
kiongozi kutoka kabila la Dani;
23 uHanieli mwana wa Efodi,
kiongozi kutoka kabila la Manase mwana wa Yosefu;
24 vKemueli mwana wa Shiftani,
kiongozi kutoka kabila la Efraimu mwana wa Yosefu;
25 wElisafani mwana wa Parnaki,
kiongozi kutoka kabila la Zabuloni;
26Paltieli mwana wa Azani,
kiongozi kutoka kabila la Isakari;
27 xAhihudi mwana wa Shelomi,
kiongozi kutoka kabila la Asheri;
28Pedaheli mwana wa Amihudi,
kiongozi kutoka kabila la Naftali.”
29 yHawa ndio watu ambao Bwana aliamuru wagawanye urithi kwa Waisraeli katika nchi ya Kanaani.

Copyright information for SwhNEN