‏ Nehemiah 12

Makuhani Na Walawi Waliorudi Na Zerubabeli

1 aHawa wafuatao walikuwa makuhani na Walawi ambao walirudi na Zerubabeli mwana wa Shealtieli pamoja na Yeshua:

Seraya, Yeremia, Ezra,
2Amaria, Maluki, Hatushi,
3Shekania, Rehumu, Meremothi,
4 bIdo, Ginethoni, Abiya,
5Miyamini, Moadia, Bilga,
6 cShemaya, Yoyaribu, Yedaya,
7 dSalu, Amoki, Hilkia na Yedaya.
Hawa walikuwa viongozi wa makuhani na wenzao wakati wa Yeshua.

8 eWalawi walikuwa Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda, na pia Matania, ambaye pamoja na wenzake, alikuwa kiongozi wa nyimbo za shukrani. 9Bakbukia na Uni, wenzao, walisimama mkabala nao wakati wa ibada.

10 fYeshua alikuwa baba wa Yoyakimu, Yoyakimu alikuwa baba wa Eliashibu, Eliashibu alikuwa baba wa Yoyada, 11Yoyada alikuwa baba wa Yonathani, na Yonathani alikuwa baba wa Yadua.

12Katika siku za Yoyakimu, kulikuwa na wakuu wa jamaa za kikuhani:

wa jamaa ya Seraya, Meraya;
wa jamaa ya Yeremia, Hanania;
13wa jamaa ya Ezra, Meshulamu;
wa jamaa ya Amaria, Yehohanani;
14wa jamaa ya Maluki, Yonathani;
wa jamaa ya Shebania, Yosefu;
15wa jamaa ya Harimu, Adna;
wa jamaa ya Meremothi, Helkai;
16 gwa jamaa ya Ido, Zekaria;
wa jamaa ya Ginethoni, Meshulamu;
17 hwa jamaa ya Abiya, Zikri;
wa jamaa ya Miniamini na ya Maazia, Piltai;
18wa jamaa ya Bilgai, Shamua;
wa jamaa ya Shemaya, Yehonathani;
19wa jamaa ya Yoyaribu, Matenai;
wa jamaa ya Yedaya, Uzi;
20wa jamaa ya Salu, Kalai;
wa jamaa ya Amoki, Eberi;
21wa jamaa ya Hilkia, Hashabia;
wa jamaa ya Yedaya, Nethaneli.
22Wakuu wa jamaa za Walawi katika siku za Eliashibu, Yoyada, Yohanani na Yadua, pia wale jamaa za makuhani, waliandikishwa wakati wa utawala wa Dario, Mwajemi. 23 iWakuu wa jamaa miongoni mwa wazao wa Lawi hadi wakati wa Yohanani mwana wa Eliashibu waliandikishwa katika kitabu cha kumbukumbu. 24 jViongozi wa Walawi walikuwa: Hashabia, Sherebia, Yeshua mwana wa Kadmieli na wenzao, waliosimama mkabala nao kusifu na kushukuru, sehemu moja ikipokezana na nyingine kama ilivyoagizwa na Daudi mtu wa Mungu.

25Mabawabu waliokuwa wakilinda kwenye malango ya ghala ni: Matania, Bakbukia, Obadia, Meshulamu, Talmoni na Akubu. 26 kWalihudumu siku za Yoyakimu mwana wa Yeshua, mwana wa Yosadaki, na katika siku za mtawala Nehemia, na za Ezra kuhani na mwandishi.

Kuwekwa Wakfu Ukuta Wa Yerusalemu

27 lWakati wa kuwekwa wakfu ukuta wa Yerusalemu, Walawi walitafutwa kule walikokuwa wakiishi, nao wakaletwa Yerusalemu kuadhimisha kwa shangwe huko kuweka wakfu kwa nyimbo za shukrani na kwa uimbaji wakitumia matoazi, vinubi na zeze. 28 mPia waimbaji walikusanywa pamoja kutoka maeneo yaliyozunguka Yerusalemu, kutoka vijiji vya Wanetofathi, 29kutoka Beth-Gilgali, na kutoka eneo la Geba na Azmawethi, kwa kuwa waimbaji walikuwa wamejijengea vijiji kuzunguka Yerusalemu. 30 nWakati makuhani na Walawi walipokuwa wamekwisha kujitakasa kwa kufuatana na desturi, waliwatakasa watu, malango na ukuta.

31 oNiliwaagiza viongozi wa Yuda wapande juu ya ukuta. Pia niliagiza makundi mawili makubwa ya waimbaji waimbe nyimbo za kumshukuru Mungu. Kundi moja lilipanda juu ya ukuta upande wa kuume, kuelekea Lango la Samadi. 32Hoshaya na nusu ya viongozi wa Yuda wakawafuata, 33pamoja na Azaria, Ezra, Meshulamu, 34 pYuda, Benyamini, Shemaya, Yeremia, 35 qpamoja na baadhi ya makuhani wenye tarumbeta, na pia walikuwa na Zekaria mwana wa Yonathani, mwana wa Shemaya, mwana wa Matania, mwana wa Mikaya, mwana wa Zakuri, mwana wa Asafu, 36 rpamoja na wenzake, Shemaya, Azareli, Milalai, Gilalai, Maai, Nethaneli, Yuda na Hanani, wakiwa na vyombo vya uimbaji, kama ilivyoagizwa na Daudi mtu wa Mungu. Mwandishi Ezra aliongoza maandamano. 37 sKwenye Lango la Chemchemi waliendelea moja kwa moja mpaka kwenye ngazi za Mji wa Daudi, kwenye mwinuko wa ukuta, na kupitia juu ya nyumba ya Daudi mpaka kwenye Lango la Maji upande wa mashariki.

38 tKundi la pili la waimbaji lilielekea upande wa kushoto. Niliwafuata juu ya ukuta, pamoja na nusu ya watu kupitia Mnara wa Tanuru mpaka kwenye Ukuta Mpana, 39 ujuu ya Lango la Efraimu, Lango la Yeshana, Lango la Samaki, Mnara wa Hananeli, na Mnara wa Mia, mpaka kwenye Lango la Kondoo. Walipofika kwenye Lango la Ulinzi wakasimama.

40 vKisha yale makundi mawili ya waimbaji yaliyoshukuru yakachukua nafasi zao katika nyumba ya Mungu. Nami pia nikafanya hivyo, pamoja na nusu ya maafisa, 41na makuhani wafuatao: Eliakimu, Maaseya, Miniamini, Mikaya, Elioenai, Zekaria na Hanania wakiwa na tarumbeta zao, 42na pia Maaseya, Shemaya, Eleazari, Uzi, Yehohanani, Malkiya, Elamu na Ezeri. Makundi haya yaliimba chini ya uongozi wa Yezrahia. 43 wSiku hiyo watu walitoa dhabihu nyingi, wakishangilia kwa sababu Mungu aliwapa furaha kuu. Wanawake na watoto walishangilia pia. Sauti ya kushangilia huko Yerusalemu iliweza kusikika mbali sana.

44 xWakati huo watu walichaguliwa kuwa wasimamizi wa vyumba vya ghala kwa ajili ya matoleo, malimbuko na zaka. Kutoka kwenye yale mashamba yaliyozunguka miji walipaswa walete kwenye ghala mafungu kama sheria ilivyoamuru kwa ajili ya makuhani na Walawi, kwa kuwa Yuda alifurahishwa na huduma ya makuhani na Walawi. 45 yWalifanya ibada ya Mungu wao na ibada ya utakaso, nao waimbaji na walinzi wa lango wakafanya hivyo pia, kufuatana na amri za Daudi na Solomoni mwanawe. 46 zMuda mrefu uliopita, katika siku za Daudi na Asafu, walikuwepo viongozi wa waimbaji na wa nyimbo za sifa na za kumshukuru Mungu. 47 aaKwa hiyo katika siku za Zerubabeli na za Nehemia, Israeli wote walitoa mafungu kila siku kwa ajili ya waimbaji na mabawabu. Pia walitenga fungu kwa ajili ya Walawi wengine, nao Walawi walitenga fungu kwa ajili ya wazao wa Aroni.

Copyright information for SwhNEN