‏ Job 17

1 aMoyo wangu umevunjika,
siku zangu zimefupishwa,
kaburi linaningojea.
2 bHakika wenye mizaha wamenizunguka;
macho yangu yamebaki kutazama uadui wao.

Ayubu Anaomba Msaada

3 c“Ee Mungu, nipe dhamana unayodai.
Ni nani mwingine atakayeweka dhamana kwa ajili yangu?
4 dUmezifunga akili zao zisipate ufahamu,
kwa hiyo hutawaacha wapate ushindi.
5 eKama mtu akiwashutumu rafiki zake ili apate ujira,
macho ya watoto wake yatashindwa kuona.

6 f“Mungu amenifanya kitu cha dhihaka kwa kila mtu,
mtu ambaye watu humtemea mate usoni.
7 gMacho yangu yamefifia kwa ajili ya majonzi;
umbile langu lote ni kama kivuli.
8 hWatu wanyofu wanatishwa na hili;
watu wasio na hatia wanasimama dhidi ya wasiomcha Mungu.
9 iHata hivyo, waadilifu watazishika njia zao,
nao wale wenye mikono safi wataendelea kupata nguvu.

10 j“Lakini ninyi njooni, ninyi nyote, jaribuni tena!
Sitampata mtu mwenye hekima miongoni mwenu.
11 kSiku zangu zimepita, mipango yangu imevunjika,
vivyo hivyo shauku za moyo wangu.
12 lWatu hawa hufanya usiku kuwa mchana,
kwenye giza wao husema, ‘Mwanga u karibu.’
13 mKama nyumba pekee ninayoitarajia ni kaburi,
Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.

kama nikikitandika kitanda changu gizani,
14 okama nikiuambia uharibifu, ‘Wewe u baba yangu,’
na kuliambia buu, ‘Wewe u mama yangu’ au ‘Dada yangu,’
15liko wapi basi tarajio langu?
Ni nani awezaye kuona tarajio lolote kwa ajili yangu?
16 pJe, litashuka chini hadi kwenye malango ya mauti?
Malango ya mauti hapa ina maana ya Kuzimu.

Je, tutashuka pamoja mavumbini?”
Copyright information for SwhNEN