Jeremiah 31
Mahamisho Kurudi Kwa Shangwe
1 a“Wakati huo, nitakuwa Mungu wa koo zote za Israeli nao watakuwa watu wangu,” asema Bwana.2 bHili ndilo asemalo Bwana:
“Watu watakaopona upanga
watapata upendeleo jangwani;
nitakuja niwape Israeli pumziko.”
3 c Bwana alitutokea wakati uliopita, akisema:
“Nimekupenda kwa upendo wa milele,
nimekuvuta kwa wema.
4 dNitakujenga tena nawe utajengeka upya,
ewe Bikira Israeli.
Utachukua tena matari yako
na kwenda kucheza na wenye furaha.
5 eUtapanda tena shamba la mizabibu
juu ya vilima vya Samaria,
wakulima watapanda
na kufurahia matunda yake.
6 fItakuja siku wakati walinzi watakapowapigia kelele
juu ya vilima vya Efraimu wakisema,
‘Njooni, twendeni juu Sayuni,
kwake Bwana Mungu wetu.’ ”
7 gHili ndilo asemalo Bwana:
“Mwimbieni Yakobo kwa furaha,
mpigieni kelele aliye mkuu wa mataifa.
Zifanyeni sifa zenu zisikike, nanyi mseme,
‘Ee Bwana, okoa watu wako,
mabaki ya Israeli.’
8 hTazama, nitawaleta kutoka nchi ya kaskazini
na kuwakusanya kutoka miisho ya dunia.
Miongoni mwao watakuwepo vipofu na viwete,
mama wajawazito na wenye utungu wa kuzaa.
Umati mkubwa wa watu utarudi.
9 iWatakuja wakilia;
wataomba wakati ninawarudisha.
Nitawaongoza kando ya vijito vya maji
katika mapito yaliyo tambarare ambapo hawatajikwaa,
kwa sababu mimi ndimi baba wa Israeli,
naye Efraimu ni mzaliwa wangu wa kwanza.
10 j“Sikieni neno la Bwana, enyi mataifa,
litangazeni katika nchi za pwani ya mbali:
‘Yeye aliyewatawanya Israeli atawakusanya
na atalichunga kundi lake la kondoo kama mchungaji.’
11 kKwa kuwa Bwana atamlipia fidia Yakobo
na kuwakomboa mkononi mwa walio na nguvu kuliko wao.
12 lWatakuja na kupiga kelele kwa furaha katika miinuko ya Sayuni;
watashangilia ukarimu wa Bwana:
nafaka, divai mpya na mafuta,
wana-kondoo wachanga
na ndama wa makundi ya ngʼombe nitakaowapa.
Watakuwa kama bustani iliyonyeshewa vizuri,
wala hawatahuzunika tena.
13 mKisha wanawali watacheza na kufurahi,
vijana waume na wazee pia.
Nitageuza maombolezo yao kuwa furaha,
nitawapa faraja na furaha badala ya huzuni.
14 nNitawashibisha makuhani kwa wingi,
nao watu wangu watajazwa kwa ukarimu wangu,”
asema Bwana.
15 oHili ndilo asemalo Bwana:
“Sauti imesikika huko Rama,
maombolezo na kilio kikubwa,
Raheli akiwalilia watoto wake
na anakataa kufarijiwa,
kwa sababu watoto wake hawako tena.”
16 pHili ndilo asemalo Bwana:
“Izuie sauti yako kulia,
na macho yako yasitoe machozi,
kwa kuwa kazi yako itapata thawabu,”
asema Bwana.
“Watarudi kutoka nchi ya adui.
17Kwa hiyo kuna tumaini kwa siku zijazo,”
asema Bwana.
“Watoto wako watarudi nchi yao yenyewe.
18 q“Hakika nimeyasikia maombolezo ya Efraimu:
‘Ulinirudi kama ndama mkaidi,
nami nimekubali kutii.
Unirudishe, nami nitarudi,
kwa sababu wewe ndiwe Bwana, Mungu wangu.
19 rBaada ya kupotea, nilitubu;
baada ya kuelewa, nilijipiga kifua.
Niliaibika na kuona haya
kwa sababu niliibeba aibu ya ujana wangu.’
20 sJe, Efraimu si mwanangu mpendwa,
mtoto ninayependezwa naye?
Ingawa mara kwa mara ninanena dhidi yake,
bado ninamkumbuka.
Kwa hiyo moyo wangu unamwonea shauku,
nina huruma kubwa kwa ajili yake,”
asema Bwana.
21 t“Weka alama za barabara,
weka vibao vya kuelekeza.
Zingatia vyema njia kuu,
barabara ile unayoipita.
Rudi, ee Bikira Israeli,
rudi kwenye miji yako.
22 uUtatangatanga hata lini,
ee binti usiye mwaminifu?
Bwana ameumba kitu kipya duniani:
mwanamke atamlinda mwanaume.”
23 vHili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo, “Nitakapowarudisha toka nchi ya kutekwa kwenu, watu walio katika nchi ya Yuda na miji yake kwa mara nyingine tena watatumia maneno haya: ‘Bwana akubariki, ee makao ya haki, ee mlima mtakatifu.’ 24 wWatu wataishi pamoja katika Yuda na miji yake yote, wakulima na wote wanaohamahama na mifugo yao. 25 xNitawaburudisha waliochoka na kuwatuliza walio na huzuni.”
26Kwa jambo hili niliamka na kuangalia pande zote. Usingizi wangu ulikuwa mtamu kwangu.
27 y Bwana asema, “Siku zinakuja, nitakapoongeza idadi ya watu, na kuzidisha hesabu ya mifugo katika nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda. 28 zKama vile nilivyowaangalia ili kungʼoa na kubomoa, kuharibu, kuangamiza na kuleta maafa juu yao, vivyo hivyo nitawaangalia ili kujenga na kupanda,” asema Bwana. 29 aa“Katika siku hizo, watu hawatasema tena,
“ ‘Baba wamekula zabibu chachu,
nayo meno ya watoto yakatiwa ganzi.’
30 abBadala yake, kila mmoja atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe; yeyote alaye zabibu chachu, meno yake mwenyewe yatatiwa ganzi.
31 ac“Siku zinakuja,” asema Bwana,
“nitakapofanya agano jipya
na nyumba ya Israeli
na nyumba ya Yuda.
32 adHalitafanana na agano
nililofanya na baba zao
wakati nilipowashika mkono
kuwaongoza watoke Misri,
kwa sababu walivunja agano langu,
ijapokuwa nilikuwa mume kwao,”
asema Bwana.
33 ae“Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli
baada ya siku zile,” asema Bwana.
“Nitaweka sheria yangu katika nia zao,
na kuiandika mioyoni mwao.
Nitakuwa Mungu wao,
nao watakuwa watu wangu.
34 afMtu hatamfundisha tena jirani yake,
wala mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Mjue Bwana Mungu,’
kwa sababu wote watanijua mimi,
tangu aliye mdogo kabisa kwao, hadi aliye mkuu sana,”
asema Bwana.
“Kwa sababu nitasamehe uovu wao,
wala sitazikumbuka dhambi zao tena.”
35 agHili ndilo asemalo Bwana,
yeye aliyeweka jua
liwake mchana,
yeye anayeamuru mwezi na nyota
kungʼaa usiku,
yeye aichafuaye bahari
ili mawimbi yake yangurume;
Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake:
36 ah“Ikiwa amri hizi zitaondoka machoni pangu,”
asema Bwana,
“ndipo wazao wa Israeli watakoma
kuwa taifa mbele yangu daima.”
37 aiHili ndilo asemalo Bwana:
“Ikiwa mbingu zilizo juu zitaweza kupimika
na misingi ya dunia chini
ikaweza kuchunguzwa,
ndipo nitakapowakataa wazao wote wa Israeli
kwa sababu ya yote waliyoyatenda,”
asema Bwana.
38 aj“Siku zinakuja,” asema Bwana, “wakati mji huu utajengwa upya kwa ajili yangu, kuanzia mnara wa Hananeli hadi Lango la Pembeni. 39 akKamba ya kupimia itaanzia hapo kuendelea hadi kwenye kilima cha Garebu, na kisha kugeuka kuelekea Goa. 40 alBonde lote watupwapo maiti na majivu pia na matuta yote kutoka Bonde la Kidroni upande wa mashariki hadi pembe ya Lango la Farasi, itakuwa takatifu kwa Bwana. Kamwe mji huu hautangʼolewa tena wala kubomolewa.”
Copyright information for
SwhNEN