‏ Isaiah 19

Unabii Kuhusu Misri

1 aNeno kuhusu Misri:

Tazama, Bwana amepanda juu ya wingu liendalo kwa haraka
naye anakuja Misri.
Sanamu za Misri zinatetemeka mbele yake,
nayo mioyo ya Wamisri inayeyuka ndani yao.

2 b“Nitamchochea Mmisri dhidi ya Mmisri,
ndugu atapigana dhidi ya ndugu,
jirani dhidi ya jirani,
mji dhidi ya mji,
ufalme dhidi ya ufalme.
3 cWamisri watakufa moyo,
na nitaibatilisha mipango yao.
Watatafuta ushauri kwa sanamu na kwa roho za waliokufa,
kwa waaguzi na kwa wale waongeao na mizimu.
4 dNitawatia Wamisri
mikononi mwa bwana mkatili
na mfalme mkali atatawala juu yao,”
asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote.

5 eMaji ya mito yatakauka,
chini ya mto kutakauka kwa jua.
6 fMifereji itanuka;
vijito vya Misri vitapungua
na kukauka.
Mafunjo na nyasi vitanyauka,
7 gpia mimea iliyoko kando ya Mto Naili,
pale mto unapomwaga maji baharini.
Kila shamba lililopandwa kando ya Mto Naili litakauka,
litapeperushwa na kutoweka kabisa.
8 hWavuvi watalia na kuomboleza,
wale wote watupao ndoano katika Mto Naili,
watadhoofika kwa majonzi.
9 iWale watu wafanyao kazi ya kitani kilichochambuliwa watakata tamaa,
wafumaji wa kitani safi watavunjika moyo.
10Wafanyao kazi ya kufuma nguo watahuzunishwa,
nao vibarua wataugua moyoni.

11 jMaafisa wa Soani ni wapumbavu kabisa,
washauri wa Farao wenye busara wanatoa ushauri wa kijinga.
Unawezaje kumwambia Farao,
“Mimi ni mmojawapo wa watu wenye hekima,
mwanafunzi wa wafalme wa zamani”?

12 kWako wapi sasa watu wako wenye hekima?
Wao wakuonyeshe na kukufahamisha
ni nini Bwana Mwenye Nguvu Zote
amepanga dhidi ya Misri.
13 lMaafisa wa Soani wamekuwa wapumbavu,
viongozi wa Memfisi
Memfisi kwa Kiebrania ni Nofu.
wamedanganyika,
walio mawe ya pembe ya taifa lake
wameipotosha Misri.
14 n Bwana amewamwagia
roho ya kizunguzungu;
wanaifanya Misri iyumbayumbe
katika yale yote inayoyafanya,
kama vile mlevi ayumbayumbavyo
katika kutapika kwake.
15 oMisri haiwezi kufanya kitu chochote,
cha kichwa wala cha mkia,
cha tawi la mtende wala cha tete.
16 pKatika siku ile Wamisri watakuwa kama wanawake. Watatetemeka kwa hofu mbele ya mkono wa Bwana Mwenye Nguvu Zote anaoinua dhidi yao. 17 qNayo nchi ya Yuda itawatia hofu Wamisri, kila mmoja atakayetajiwa Yuda ataingiwa na hofu, kwa sababu ya kile ambacho Bwana Mwenye Nguvu Zote anapanga dhidi yao.

18 rKatika siku hiyo miji mitano ya Misri, itazungumza lugha ya Kanaani, na kuapa kumtii Bwana Mwenye Nguvu Zote. Mji mmojawapo utaitwa Mji wa Uharibifu.
Yaani Heliopoli (Mji wa Jua).


19 tKatika siku hiyo patakuwepo madhabahu ya Bwana katikati ya Misri na mnara wa kumbukumbu kwa Bwana kwenye mpaka wa Misri. 20 uItakuwa alama na ushahidi kwa ajili ya Bwana Mwenye Nguvu Zote katika nchi ya Misri. Watakapomlilia Bwana kwa sababu ya watesi wao, Mungu atawapelekea mwokozi na mtetezi, naye atawaokoa. 21 vHivyo Bwana atajijulisha mwenyewe kwa Wamisri, nao katika siku hiyo watamkubali Bwana. Wataabudu kwa kumtolea dhabihu na sadaka za nafaka, watamwekea Bwana nadhiri na kuzitimiza. 22 wBwana ataipiga Misri kwa tauni; atawapiga na kuwaponya. Watamgeukia Bwana, naye atayasikia maombi yao na kuwaponya.

23 xKatika siku hiyo kutakuwepo na njia kuu kutoka Misri hadi Ashuru. Waashuru watakwenda Misri, na Wamisri watakwenda Ashuru. Wamisri na Waashuru wataabudu pamoja. 24 yKatika siku hiyo Israeli itakuwa ya tatu, pamoja na Misri na Ashuru, nao watakuwa baraka kwa dunia. 25 zBwana Mwenye Nguvu Zote atawabariki, akisema, “Baraka iwe kwa Misri watu wangu, kwa Ashuru kazi ya mikono yangu, na kwa Israeli urithi wangu.”

Copyright information for SwhNEN