‏ Psalms 100

Dunia Yote Yaitwa Kumsifu Mungu

Zaburi ya shukrani.

1 aMpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote.
2 bMwabuduni Bwana kwa furaha;
njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.
3 cJueni kwamba Bwana ndiye Mungu.
Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake;
sisi tu watu wake,
kondoo wa malisho yake.

4 dIngieni malangoni mwake kwa shukrani
na katika nyua zake kwa kusifu,
mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.
5 eKwa maana Bwana ni mwema
na upendo wake wadumu milele;
uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.
Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.