‏ Isaiah 7

Ishara Ya Imanueli

1 aWakati Ahazi mwana wa Yothamu, mwana wa Uzia, alipokuwa mfalme wa Yuda, Mfalme Resini wa Aramu,
Yaani Shamu.
na Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli walipanda kupigana dhidi ya Yerusalemu, lakini hawakuweza kuushinda.

2 cWakati huu nyumba ya Daudi iliambiwa, “Aramu wameungana na Efraimu.” Kwa hiyo mioyo ya Ahazi na watu wake ilitikiswa, kama miti ya msituni inavyotikiswa na upepo.

3 dNdipo Bwana akamwambia Isaya, “Toka uende, wewe na mwanao Shear-Yashubu,
Shear-Yashubu maana yake Mabaki Watarudi.
mkutane na Ahazi huko mwisho wa mfereji wa Bwawa la Juu, kwenye barabara iendayo Shamba la Dobi.
4 fMwambie, ‘Uwe mwangalifu, utulie na usiogope. Usife moyo kwa ajili ya watu hawa wawili walio kama visiki vya kuni vifukavyo moshi, kwa ajili ya hasira kali ya Resini na Aramu na ya mwana wa Remalia. 5 gAramu, Efraimu na mwana wa Remalia wamepanga shauri baya ili wakuangamize, wakisema, 6 h“Tuishambulie Yuda, naam, tuirarue vipande vipande na kuigawa miongoni mwetu, na kumtawaza mwana wa Tabeeli awe mfalme juu yake.” 7 iLakini Bwana Mwenyezi asema hivi:

“ ‘Jambo hili halitatendeka,
halitatokea,
8 jkwa kuwa kichwa cha Aramu ni Dameski,
na kichwa cha Dameski ni Resini peke yake.
Katika muda wa miaka sitini na mitano,
Efraimu atakuwa ameharibiwa
kiasi kwamba hataweza tena kuwa taifa.
9 kKichwa cha Efraimu ni Samaria,
na kichwa cha Samaria
ni mwana wa Remalia peke yake.
Kama hamtasimama thabiti katika imani yenu,
hamtaimarika kamwe.’ ”
10 Bwana akasema na Ahazi tena, 11 l“Mwombe Bwana Mungu wako ishara, iwe kwenye vina virefu sana, au kwenye vimo virefu sana.”

12 mLakini Ahazi akasema, “Sitaomba; sitamjaribu Bwana.”

13 nNdipo Isaya akasema, “Sikia sasa, ewe nyumba ya Daudi! Je, haitoshi kujaribu uvumilivu wa wanadamu? Je, mtaujaribu uvumilivu wa Mungu wangu pia? 14 oKwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara: Bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, na ataitwa Imanueli.
Imanueli maana yake Mungu yu pamoja nasi.
15 qAtakula jibini na asali atakapokuwa ameweza kukataa mabaya na kuchagua mema. 16 rLakini kabla mtoto hajajua kukataa mabaya na kuchagua mema, nchi ya wafalme hao wawili unaowaogopa itafanywa ukiwa. 17 sBwana ataleta juu yako, juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako wakati ambao haujawahi kuwako tangu Efraimu alipojitenga na Yuda: yeye atawaleteeni mfalme wa Ashuru.”

18 tKatika siku ile Bwana atawapigia filimbi mainzi kutoka vijito vya mbali vya Misri, na nyuki kutoka nchi ya Ashuru. 19 uWote watakuja na kukaa kwenye mabonde yenye miteremko, na kwenye nyufa za miamba, kwenye vichaka vyote vyenye miiba, na kwenye mashimo yote ya maji. 20 vKatika siku ile Bwana atatumia wembe ulioajiriwa kutoka ngʼambo ya Mto,
Yaani Frati.
yaani mfalme wa Ashuru, kunyoa nywele za kichwa chako na malaika ya miguu yako, na kuziondoa ndevu zako pia.
21 xKatika siku ile, mtu atahifadhi hai ndama mmoja na kondoo wawili. 22 yKwa ajili ya wingi wa maziwa watakayotoa, atapata jibini ya kula. Wote watakaobakia katika nchi watakula jibini na asali. 23 zKatika siku ile, kila mahali palipokuwa na mizabibu elfu moja yenye thamani ya shekeli 1,000
Shekeli 1,000 ni kama kilo 11.5.
za fedha, patakuwa na michongoma na miiba tu.
24 abWatu watakwenda huko wakiwa na upinde na mshale, kwa maana nchi itafunikwa na michongoma na miiba. 25 acKuhusu vilima vyote vilivyokuwa vikilimwa kwa jembe, hamtakwenda huko tena kwa ajili ya hofu ya michongoma na miiba. Patakuwa mahali ambapo ngʼombe wataachiwa huru, na kondoo kukimbia kimbia.

Copyright information for SwhNEN