‏ Habakkuk 3

Maombi Ya Habakuki

1Sala ya nabii Habakuki iliyoimbwa kwa shigionothi.
Ni kifaa cha uimbaji chenye nyuzi; pia maombi kutumia kifaa hiki.


2 b Bwana, nimezisikia sifa zako;
nami naogopa kwa matendo yako, Ee Bwana.
Fufua kazi yako katikati ya miaka,
katikati ya miaka tangaza habari yako;
katika ghadhabu kumbuka rehema.

3 cMungu alitoka Temani,
yeye Aliye Mtakatifu kutoka Mlima Parani.
Utukufu wake ulifunika mbingu,
na sifa zake zikaifunika dunia.
4 dMngʼao wake ulikuwa kama jua lichomozalo;
mionzi ilimulika kutoka mkononi mwake,
ambako nguvu zake zilifichwa.
5 eTauni ilimtangulia;
maradhi ya kuambukiza yalifuata nyayo zake.
6 fAlisimama, akaitikisa dunia;
alitazama, na kuyafanya mataifa yatetemeke.
Milima ya zamani iligeuka mavumbi
na vilima vilivyozeeka vikaanguka.
Njia zake ni za milele.
7 gNiliona watu wa Kushani katika dhiki,
na makazi ya Midiani katika maumivu makali.

8 hEe Bwana, uliikasirikia mito?
Je, ghadhabu yako ilikuwa dhidi ya vijito?
Je, ulighadhibikia bahari
ulipoendesha farasi wako
na magari yako ya ushindi?
9 iUliufunua upinde wako
na kuita mishale mingi.
Uliigawa dunia kwa mito;
10 jmilima ilikuona ikatetemeka.
Mafuriko ya maji yakapita huko;
vilindi vilinguruma
na kuinua mawimbi yake juu.

11 kJua na mwezi vilisimama kimya mbinguni
katika mngʼao wa mishale yako inayoruka,
na katika mngʼao wa mkuki wako umeremetao.
12 lKwa ghadhabu ulipita juu ya dunia,
na katika hasira ulikanyaga mataifa.
13 mUlikuja kuwaokoa watu wako,
kumwokoa uliyemtia mafuta.
Ulimponda kiongozi wa nchi ya uovu,
ukamvua toka kichwani hadi wayo.
14 nKwa mkuki wake mwenyewe ulitoboa kichwa chake
wakati mashujaa wake walifurika nje kwa kishindo kututawanya,
wakifurahi kama walio karibu kutafuna
wale wanyonge waliokuwa mafichoni.
15 oUlikanyaga bahari kwa farasi wako,
ukisukasuka maji makuu.

16 pNilisikia na moyo wangu ukagonga kwa nguvu,
midomo yangu ikatetemeka kwa hofu niliposikia sauti;
uchakavu ukanyemelea mifupa yangu,
na miguu yangu ikatetemeka.
Hata hivyo nitasubiri kwa uvumilivu siku ya maafa
kuyajilia mataifa yaliyotuvamia.
17 qIngawa mtini hauchanui maua
na hakuna zabibu juu ya mizabibu,
ingawaje mzeituni hauzai,
na hata mashamba hayatoi chakula,
iwapo hakuna kondoo katika banda,
wala ngʼombe katika zizi,
18 rhata hivyo nitashangilia katika Bwana,
nitamfurahia Mungu Mwokozi wangu.

19 s Bwana Mwenyezi ni nguvu yangu;
huifanya miguu yangu kama miguu ya ayala,
huniwezesha kupita juu ya vilima.

Kwa kiongozi wa uimbaji. Kwa vinanda vyangu vya nyuzi.
Copyright information for SwhNEN